Kahindo Kangitse |
Kahindo Kangitse ni mmoja wa wanawake ambao wamepitia udhalilishaji wa kubakwa, lakini adha hiyo haikuishia hapo kwani mume wake alimkataa baada ya kubakwa. Na nyumbani kwao familia yake haikusaidia kwani alipata mimba kutokana na kubakwa na alipojifungua mtoto familia yake ilimtaka Kahindo amwondoe mtoto na kumrudisha kwa wanajeshi waliombaka.
Lakini uchungu wa mwana ajua mzazi, Kahindo anaendelea kumtunza mtoto wake na anapata msaada katika kituo cha taasisi isiyo ya kiserikali ambayo inasaidia watu walioathirika na vitendo vya ubakaji. Wito mkubwa wa Kahindo kwa serikali ni kwamba ihakikishe vitendo vya ubakaji vinamalizika kote DRC.