Vitendo vya ubakaji Congo havichagui watu wazima wala watoto.
Miongoni mwa waathirika wa ubakaji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni wasichana wadogo wa umri chini ya miaka 15. Ripoti kutoka vituo kadha vinavyohudumia waathirika zinasema idadi ya wasichana wadogo wanaobakwa iliongezeka katika kipindi cha mwaka 2009 na matukio ya ubakaji katika vijiji kadha 2010.
Msichana wa miaka 13, Elisa (si jina lake halisi) alibakwa wakati anaelekea nyumbani kutoka shamba. Alizungumza katika hospitali kuu ya Lubero, Kivu Kaskazini ambako alikuwa amejifungua baada ya kupata mamba alipobakwa na mtu mmoja aliyekuwa na silaha